Kesi ya Viongozi Wakuu, Wabunge CHADEMA yahairishwa kisa Esther Bulaya

Kesi ya Viongozi Wakuu, Wabunge CHADEMA yahairishwa kisa Esther Bulaya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kuanza kusikilizwa kwa ushahidi katika kesi ya namba 112 ya mwaka 2018 inayowakabili baadhi ya Viongozi Wakuu wa Chama na Wabunge 7 wa CHADEMA hadi Aprili 16 na 17 mwaka huu baada ya mshtakiwa namba 9, Esther Bulaya kutokuwepo mahakamani kwa sababu za kiafya.

Kuahirishwa kwa kesi hiyo iliyokuwa imepangwa kuendelea leo na kesho (Machi 28 na 29) kwa mashahidi wa upande wa mashtaka kuanza kutoa ushahidi, kumefuatia mabishano ya hoja za kisheria na baadae makubaliano ya pande zote mbili, mashtaka na utetezi, juu ya kuendelea na kesi hiyo huku mshtakiwa huyo akiwa hayupo mahakamani na mahakama hiyo haijapokea uthibitisho wa kimaandishi wa kauli yake kuwa ameridhia mahakama iendelee na shauri hilo bila yeye kuwepo.

Awali ilielezwa mahakamani hapo na mdhamini wa Bulaya kuwa mshtakiwa huyo ambaye ni Mbunge wa Bunda mjini ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu anaendelea na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji.

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa upande wa mashtaka na utetezi, Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo, aliahirisha kesi hiyo akiamuru kuwa itaendelea Aprili 16 na 17 saa nne asubuhi, kwa ama mshtakiwa huyo kuwepo mahakamani au mahakama kuwa na uthibitisho wa kimaandishi kutoka kwake kuwa anaridhia kesi kuendelea bila yeye kuwepo mahakamani.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad