Kadhalika imemuonya shahidi wa kwanza Mrakibu Msaidizi (ASP), Shamila Mkoma kufika mahakamani hapo Aprili 9,mwaka huu kutoa ushahidi dhidi ya Zitto.
Amri hiyo imetolewa leo na Mahakama hiyo iliyokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili wa Serikaki Wankyo Simon amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikiliza ushahidi na Jamhuri imeita shahidi mmoja ASP Mkoma.
Hata hivyo, amedai kuwa mshtakiwa hayupo mahakamani, Wakili wa utetezi, Steven Mwakibolwa amedai kuwa amepata taarifa kutoka kwa shemeji wa mshtakiwa Vicent Kasala kwamba Zitto ni mgonjwa lakini hafahamu mahali alipo.
"Kasala amenieleza kwamba mkewe Zitto kampigia kumfahamisha kwamba ni mgonjwa lakini hajui yuko wapi" amedai Nwakibolwa.
Hakimu amehoji wakili amepewa taarifa kwamba mshtakiwa ni mgonjwa lakini hana uhakika.
"Umepewa taarifa kwamba mshtakiwa anaumwa lakini huna uhakika, tusitafutane maneno hapa, siku ya kesi wadhamini na mshtakiwa waje hapa mahakamani kujieleza kwanini hawakufika mahakamani" amesema Hakimu Shaidi.
Amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri Aprili 9, mwaka huu na shahidi afike siku hiyo.