Kijiji Kilichokosa Umeme Toka Uhuru Chapata Umeme
0
March 31, 2019
Waziri wa Nishat Dkt Medad Kalemani amewasha umeme kwenye Kijiji na Shule ya Msingi katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ambapo toka nchi ilikuwa imepata uhuru hadi sasa wananchi hao walikuwa hawaja wahi kupatiwa huduma ya umeme.
Uzinduzi huo wa kuwasha umeme wa Rea wa awama ya tatu katika Wilaya ya Tanganyika ulifanyika jana katika vijiji vya Ifukutwa na Mchakamchaka katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.
Akizungumza na wananchi wa vjiji hivyo mara baada ya uzindizi wa kuwasha umeme Waziri Kaleman alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme
Hivyo aliwataka wakazi wa Mkoa wa Katavi kutumia furusa hiyo kwa kuingiza umeme huo wa rea kwa bei nafuu ya Tshs 27,000 tuu na kusisitiza wananchi wa vijijini wasitozwe zaidi ya kiasi hicho cha fedha.
Alisema mradi wa Rea awamu ya atu utakao vifikia vijiji vyote 177 vya Mkoa wa Katavi Wizara imepanga na itahakikisha unakamilika kwa muda uliopangwa na wala mkandarasi hataongezewa muda mwingine zaidi .
Alisitaka taasisi kuhakikisha zinaingiza umeme huo ili ziweze kuwahudumia wananchi kwa muda wote pasikukuwepo na kisingizio cha kukosa umeme kwani watanzania wanacho hitaji ni kupatiwa huduma .
Waziri Keleman alisema kuwa maeneo yoye yenye machimbo ya madini nayo yamepangwa kufikiwa na umeme uli wachimbaji waweze kuweka mitambo yao na kuitumia hali ambayo itawafanya waweze kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla .
Tags