Kocha wa Simba afunguka haya kuhusu Stand United

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbegiji, Patrick Aussems amesema kuwa kikosi chake kimekwenda mkoani humo kwa kazi moja ya kuchukua pointi tatu. Kocha huyu amefunguka hayo wakati timu ya Simba wakiwasili Shinyanga.

 Hata hivyo mabingwa hao watetezi watamkosa mshambuliaji wao wa kimataifa kutoka Uganda, Emmanuel Okwi ambaye ni majeruhi lakini ikielezwa kuwa beki, Erasto Nyoni yuko "fiti".

Kocha huyu alienda mbali zaidi na kusema kuwa watashuka uwanjani huku wakiwaheshimu Stand United kama timu nyingine alizokutana nazo kwenye ligi hiyo.

"Tumewafuata Stand United, tunajua kila timu sasa inajiandaa kuonyesha ushindani itakapocheza na sisi, tunajua hilo, lakini mipango yangu ni kuhakikisha tunashinda mechi hii ya Jumapili, tuko tayari," alisema Aussems.

Stand United inatarajia kuwakaribisha Simba katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM, Kambarage kuanzia saa 10:00 jioni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad