Kuhusu Mpango wa Kuanzishwa Chuo Kikuu cha Anga Tanzania

Kuhusu Mpango wa Kuanzishwa Chuo Kikuu cha Anga Tanzania
Imeripotiwa kuwa mpango wa Uanzishwaji wa chuo kikuu cha Anga Tanzania katika aneo la kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro KIA kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha shirika la ndege nchini Tanzania kwa kuwa na marubani wake wenyewe ambao watapata mafunzo hapa hapa nchini kwa gharama nafuu tofauti na ilivyo sasa.
.
Kwa mudu mrefu tangu Tanzania ipate uhuru, kumekuwa hakuna chuo kikuu cha taaluma ya Urubani, hali ambayo imewalazimu wale wote wenye nia na kujifunza taaluma hiyo kwenda nje ya nchi, lakini baada ya jitihada za serikali ya awamu ya tano za kufufua shirika la ndege, muhimu jitihada hizo zikaenda sambamba na Uanzishwaji wa chuo kikuu cha masuala ya Anga.
.
Chuo hicho ambacho kitakuwa sehemu ya Chuo cha taifa cha usafirishaji NIT kimependekezwa kujengwa katika eneo la uwanja wa KIA kutokana na miundombinu muhimu ya mafunzo kwa vitendo pamoja na eneo la kutosha ambapo tayari zaidi ya hekta 60 zimesha tengwa na uongozi wa KIA kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine muhimu kwa ajili ya Chuo hicho.
.
Tayari baadhi ya wabia muhimu katika mpango huu likiwemo taifa la China na Afrika ya Kusini wamefika katika eneo la KIA kwa ajili ya ukaguzi wa awali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chuo kikuu cha kwanza cha mafunzo ya urubani chini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad