Kukamatwa Wabunge wa Upinzani, Msajili wa Vyama atwishwa zigo

Kukamatwa Wabunge wa Upinzani, Msajili wa Vyama atwishwa zigo
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametakiwa kutoa tamko kuhusu kamatakamata ya wabunge wa upinzani inayoendelea nchini kwa sasa.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Katibu Mkuu wa Chama cha Ada-Tadea, John Shibuda ambaye amesema kauli yake kuhusu suala hilo huenda ikasababisha chama husika kumgeuka, hivyo kuna haja suala hilo kutolewa tamko na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kuwa ndiye mlezi wa vyama nchini.

"Mimi siwezi 'nika-react' au kutoa 'statement' (tamko) bila chama husika 'ku-appeal' (kukata rufani) kwa sababu naweza nikafanya hivyo, halafu chama kikanigeuka kwamba nisiingilie mambo yao, ila msajili pia anatakiwa atoe 'statement' kwa kuwa ndiye mlezi wetu," Shibuda alisema.

Hivi karibuni, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, aliitwa polisi kwa madai ya kutenda kosa la uchochezi.

Wiki iliyopita, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu (Chadema), alikamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa lugha ya uchochezi kuhusiana na suala la vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo vilivyotolewa na serikali hivi karibuni.

Juzi, wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali na Suzan Kiwanga (wote wa Morogoro), walikamatwa na kuwekwa mahabusu na kusomewa upya mashtaka ya kudaiwa kuchoma moto ofisi ya kijiji wakati wa uchaguzi mdogo ambayo awali yalifutwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad