Queen Darleen akana kumtelekeza baba yao


Dada wa msanii wa muziki wa bongo fleva Diamond Platnumz, Queen Darleen amefunguka na kukanusha taarifa ambazo zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kumtelekeza baba yao akiwa mgonjwa.

Akiongea na Wasafi TV, Darleen amesema kuwa picha hizo mbaya za mzee huyo ambazo zinasambaa mitandaoni ni za zamani sana.

“Mzee tunampigia simu na kuzungumza naye mara kwa mara lakini sasa yeye anachokitaka uende na ukifika atakutembeza kwa marafiki zake wote sasa ni kitu ambacho hakiwezekani. Na zile picha anaonekana anaumwa nizatoka mwaka 2015, mwenyewe nilivyoziona nilishituka na nilichukia sana,” alisema Darleen.

Queen Darleen alienda mbali zaidi na kusema kuwa  “Baba ni mtu ambaye alikuwa na hela, lakini hela yake mwenyewe kaitumia na imekwisha hata nikampatia ya kwangu haitaweza mtosha. Kwa hiyo pale tunapojaaliwa kumpa tunampatia, hatuwezi ‘kufosi’jamii kiambia baba yetu sisi tunamfanyaia hichi na hichi,”

Wiki iliyopita katika mitandao ya kijamii zilikuwa zinasambaa video zikimuonyesha mzee huyo akilalamika huku akidai kwa sasa ni mgonjwa na anahitaji msaada.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad