Lipumba Amshangaa Lowassa Kurudi CCM Mbowe akiwa Gerezani

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema anashangazwa na uamuzi wa Edward Lowassa kurejea CCM katika kipindi ambacho mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa gerezani.

Akihojiwa na Gazeti la Mwananchi,  Profesa Lipumba, ambaye mwaka 2015 alijivua uenyekiti kutokana na CUF kuunga mkono Lowassa kugombea urais kwa mgongo wa vyama vinne, amesema hajashangazwa na hatua ya Lowassa kurejea CCM kwa kuwa alijua ingawa hakufahamu siku.

"Lowassa amerudi CCM bila aibu wakati Mbowe bado yupo gerezani. Hakufikiria wenzake anawaachaje," amesema Profesa Lipumba.

Lipumba amesema ni vyema wapinzani wakawa na msimamo na kwamba mapambano ya kudai haki yanahitaji muda mrefu si harakaharaka kama walivyofanya Chadema kumchukua Lowassa ili awasaidie kuchukua nchi.

"Niliwaambia Lowassa amekuja upinzani kwa ajili ya madaraka tu. Hiki cha leo ni dhambi ya usaliti waliomfanyia (katibu wa zamani wa Chadema, Willbrod) Dk Slaa inaanza kuwatafuna,” alisema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad