Lissu Atoa ya Moyoni Kuhusu Lowasa Kurudi CCM

Baada ya ushindi, Zahera awachana wachezaji
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amezungumzia matokeo pamoja na kiwango ambacho klabu yake imekionesha katika mchezo dhidi ya Alliance akisema kuwa kuna vitu vingi haviko sawa.



Akizungumza na www.eatv, akiwa njiani kurejea Dar es salaam kutoka mkoani Mwanza ambako Yanga ilicheza na Alliance FC na kupata ushindi wa bao 1-0 bao lililofungwa na Amisi Tambwe, kocha Zahera amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mchezo huo aliwapongeza wachezaji wake lakini kuna vitu haviko sawa na hakuna haja ya kuvieleza katika mikutano na wanahabari.

"Mechi ilipomalizika nikawaambia wachezaji wangu hongera, ila tutasimuliana mazoezini jinsi ilivyokuwa kwasababu kuna vitu sikufurahi navyo kutokana na wachezaji wenyewe hawakuheshimu mtego tulioutayarisha", amesema Zahera. 

"Nadhani nyinyi waandishi wengi mtaniuliza ni wachezaji gani awa kufuata plani yangu,  kuna wachezaji wawili ila siyo lazima niwapatie majina yao, wao wenyewe  wameshajijua. Nitawaambia timu nzima ili kuwaonesha kuwa kama kunakuwa na mpango maalumu basi tunapaswa kuukamilisha sisi wote", ameongeza kocha huyo.

Katika msimamo wa ligi, Yanga inaongoza ikiwa na pointi 64 katika mechi 26 ilizoshuka dimbani mpaka sasa, Azam FC ikiwa katika nafasi ya pili kwa pointi 53 huku Simba ikiendelea kusali katika nfasi ya tatu kwa pointi 51 baada ya kucheza michezo 20.

Yanga inatarajia kurejea Dar es salaam kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya KMC, mchezo utakaopigwa Machi 10.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad