Aliyewahi kuwa kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kuwa staili ya uchezaji wa klabu hiyo haijabadilika chini ya Ole Gunnar Solskjaer.
Aliyewahi kuwa kocha wa Manchester United, Louis van Gaal
Wakati vyombo vya habari vikiripoti siku ya Jumatatu kuwa Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kukabidhiwa jumla jumla United kwa kandarasi ya muda mrefu Van Gaal ameibuka na kusema hakuna mabadiliko ya kiuchezaji ndani ya timu hiyo.
Solskjaer mwenye umri wa miaka 46, ameshinda jumla ya michezo 14 kati ya mechi 19 tangu kukabidhiwa timu hiyo mwezi Desemba akirithi mikoba ya Jose Mourinho.
Van Gaal, ambaye naye alipitia wakati mgumu akiwa Old Trafford kama ilivyo kwa Mourinho amesema kuwa Solskjaer amefanikiwa lakini anaamini aina ya uchezaji ndani ya klabu hiyo ya kupaki basi haija badilika.
”Kocha aliyenifuatia baada yangu mimi ambaye alikuwa Mourinho alibadilisha staili ya kupaki basi na badala yake ikawa ‘counter’,” Mholanzi huyo ameiyambia BBC.
”Kwa sasa kuna kocha ambaye anapaki basi na kucheza ‘counter’ tofauti kubwa iliyopo kati ya Mourinho na Solskjaer ni kwamba Solskjaer anashinda.”
”Mimi sipo pale, lakini hali inaonekana imetulia kwa sasa na mazingira yamekuwa mazuri. Ukweli ni kwamba Solskjaer amembadilisha, Paul Pogba katika eneo alilokuwepo mwanzo na kumueka sehemu muhimu zaidi.”
”Lakini namna Manchester United inavyocheza kwa sasa ni tofauti na ilivyokuwa ikicheza kwa Sir Alex Ferguson. Inacheza mpira wa kujilinda na kushambulia, kama utapenda penda.”
Van Gaal anaamini kuwa Solskjaer anayonafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya Champions League na pointi ya kuzingatia ni kwamba kama atafanikiwa kwenye hilo itamdharaulisha Mourinho.
”Anaweza kutwaa taji la Champions League kwa sababu anacheza mfumo wa kujilinda ambao ni ngumu sana kufungwa iwe unapenda hilo ama hupendi na ni matokeo ya kazi ya Mourinho.
United imezidiwa pointi mbili na Arsenal yenye alama 60 inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Premier League huku ikitarajiwa kukutana na Barcelona hatua ya robo fainali ya Champions League mwezi ujao.