Maalim Seif Amjibu Msajili wa Vyama

Maalim Seif Amjibu Msajili wa Vyama
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, amesema sheria aliyotumia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuwaonya waliokuwa wanachama wa chama hicho waliochoma bendera na kadi za chama hicho, haipo.

Maalim Seif amesema hayo leo Jumatano Machi 20, wakati akihojiwa na Maria Sarungi katika mtandao wa Kwanza TV, akirejea tamko la Jaji Mutungi alilolitoa jana akiwaonya wanachama hao waliohamia Chama cha ACT-Wazalendo, pamoja Maalim Seif.

“Msajili anasema tumevunja sheria, sheria ipi, tunavyojua kuna sheria iliyopitishwa lakini hadi sasa hatuna hakika kama rais ameweka saini maana utaratibu ni kwamba kama amesaini ingewekwa kwenye gazeti la serikali lakini hadi sasa hakuna gazeti la serikali lililochapisha sheria hiyo.

“Sasa msajili anatumia sheria ipi ambayo ameirejea kifungu chake au anayo yeye peke yake?” amehoji Maalim Seif.

Aidha, Maalim Seif amesema ni kama vile dola inawatega wananchi wake kwa sababu haiwezekani kutumia sheria ambayo wananchi wake hawaijui.

“Kwanza tunauliza ni sheria ipi labda anayosema kwenye kupandisha bendera kuna maneno wanayatamka, wanasema Alah Akbar maana yake Mungu Mkubwa, lakini kwa upande wa wakristo wangekuwa wanapandisha bendera wanasema Bwana Asifiwe, angeuliza?

“Lakini isitoshe katika baadhi ya mikutano ya CCM (Chama Cha Mapinduzi), wanaanza kwa kusoma Quraan, sasa hii inakuja kwa ajili ya Cuf tu au vyama vingine, mimi namuomba msajili sana awe ‘fair’ maana unapokuwa na mamlaka ya kuamua uache mapenzi na chuki,” amesema Maalim Seif.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad