Majaji Wapendekeza Umri Kufanya Ngono Uwe Miaka 16 Badala ya 18

Majaji Wapendekeza Umri Kufanya Ngono Uwe Miaka 16 Badala ya 18
MAHAKAMA ya Rufaa nchini Kenya imependekeza umri wa kuruhusiwa kujihusisha na ngono nchini Kenya upunguzwe kwa miaka miwili.

Kwa sasa, sheria za Kenya zinaruhusu vijana wa miaka 18 na kuendelea kufanya ngono. Gazeti binafsi la The Standard la nchini Kenya linaripoti kuwa majaji watatu wa mahakama hiyo wamependekeza maboresho ya sheria na umri wa kuruhusiwa kufanya ngono ushushwe kutoka miaka 18 mpaka 16.

 Gazeti hilo linadai kuwa majaji hao wanapingana na adhabu kali ya vifungo virefu jela wanayopewa vijana wa kiume kwa “kushiriki ngono na mabinti ambao tayari ama wanataka kuwa wakubwa.”

 Majaji hao wametumia mfano wa kesi moja ambayo walitupilia mbali kifungo cha mika 15 alichopatiwa mwanamme mmoja kwa kumtia mimba msichana wa miaka 17.

Pia wanadai kuwa baadhi ya wavulana na wasichana walio chini ya miaka 18 wanajihusisha na mahusiano ya kingono “wakiwa macho meupe kabisa (wakijua wafanyayo),” linaripoti gazeti hilo.

 “Magereza yetu yamejaa na vijana wa kiume ambao wanatumikia vifungo virefu kwa kushiriki ngono na wasichana ambao ridhaa yao ya kufanya matendo hayo haitambuliki kisheria sababu tu hawajafikia miaka 18,” majaji hao wamekaririwa wakisema.

“Yawezekana hawajafikia umri wa utu uzima lakini yawezekana tayari wameshafikia umri wa kuridhia kufanya ngono, na wanaweza kuchukua hatua sahihi na za kiweledi kuhusu maisha yao na miili yao,” alisema mmoja wao.

 Katika kesi husika, Eliud Waweru alifungwa baada kumtia mimba msichana ambaye alikuwa amemaliza kidato cha nne.
Majaji Wapendekeza Umri Kufanya Ngono Uwe Miaka 16 Badala ya 18


Waweru kabla ya hapoalipatana na baba wa binti huyo kuwa atalipa mahari ya KSh80,000 baada ya kutoroka na mpenzi wake huyo. ambapo alikamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kushindwa kulipa mahari hiyo.

Majaji wamesema kuwa msichana huyo alilazimishwa kutoa ushahidi dhidi ya Waweru na wazazi wake, jambo ambalo aliliandika kwenye barua zake mbili na kutishia kujiua. Waweru ambaye ametumikia miaka minane ya kifungo hicho ameachiliwa huru Ijumaa iliyopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad