Majambazi watano wauawa Dar es Salaam

Majambazi watano wauwa Dar es Salaam
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua majambazi watano na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne, kukamata silaha nne na risasi 59 katika matukio  matatu tofauti.

Marchi 3 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili na  nusu jioni huko maeneo ya Kibaha Maili moja Jeshi la Polisi likiwa katika ufuatiliaji lilimkamata mtuhumiwa moja aitwaye Friday Samson  (29)askari wa JWTZ Kikosi cha 36KJ Kibaha Msangani na katika mahojiano ya kina alikiri kumiliki silaha mbili kinyume cha sheria na kwamba huzihifadhi silaha hizo nyumbani kwa mke mdogo mtaa wa Muheza Kibaha Pwani  na hufanyia matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali.

Baada ya mahojiano Jeshi la Polisi pamoja na mtuhumiwa huyo walifika kwenye nyumba hiyo na kufanikiwa  kukamata  silaha aina ya AK 47 yenye namba NM174844 ikiwa na risasi 20 ndani ya magazine, boksi moja likiwa na risasi 27,bastola moja yenye namba 3249 ikwa na risasi 7 ndani ya magazine na risasi 3 za silaha ya G3.

Mtuhumiwa alikubali kuwaonyesha wenzake watatu anaoshirikiana nao katika matukio hayo na askari walipofika kwenye nyumba wanayoishi watuhumiwa hao walianza kukimbia kupitia mlango wa nyuma na hatimaye askari walirusha risasi hewani kuwaamuru wasimame lakini walikaidi na ndipo walipowafyatulia risasi za miguu ambazo ziliwajeruhi na walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa  hospitali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad