Makonda Amkabidhi Milioni Moja kijana Aliyetoka Manyara kwa Baiskeli Kushangilia Stars

Makonda Amkabidhi Milioni Moja kijana Aliyetoka Manyara kwa Baiskeli Kushangilia Stars
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi pesa taslim kiasi cha shilingi Milioni moja kijana Ikuzi Kicheko ambaye alifunga safari kutoka Mkoa wa Manyara hadi Dar es Salaam akitembea kwa biskeli kwa ajili ya kuhamasisha watu kujitokeza katika uwanja wa Taifa kuisapoti timu ya TAIFA STARS ilipokuwa ikicheza na timu ya taifa ya Uganda, Jumapili, Machi 24, 2019.



RC Makonda amesema kitendo alichokifanya kijana huyo ni cha kizalendo na kutoa wito kwa Watanzania wengine kujitokeza kuisapoti timu yetu ya taifa kwa njia yoyote ile.



Akizungumza kijana huyo amesema alipofika Dar es Salaam, alizunguka katika katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuanzia Kariakoo, Posta, Makumbusho, Mwenge na sehemu zingine akihamasisha Watanzania kujitokeza kuishabikia Stars.



“Wapo walioniona kama ni chizi, wngine walisema ninavuta bangi lakini pia wapo ambao walitambua umhimu wa ninachokifanya, walisimamisha magari yao na kunipa shilingi 2000, na kunitia moyo niendle kuhamasisha,” alisema Kicheko.



Aidha, viongozi wa TFF wameahidi kumpatia zawadi zaidi na kwa kuanzia wamempa nguo zikiwemo Jezi Original za Taifa Stars na mpira ili akirudi Mkoani Manyara watu wasimshangae na kumkataa tena njiani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad