Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameahidi kuwasomesha watoto wa kike 100 waliofaulu vizuri mitihani ya kidato cha nne, hivyo atawasomesha kidato cha tano na sita.
Akizungumza mbele ya maelfu ya akina mama waliojitokeza katika siku ya mahadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam, Makonda amesema watoto wao ni wale ambao familia zao ni za chini pamoja na yatima.
"Ndani ya Mkoa wa Dar es salaam tumefanikiwa kuwasaidia watoto 1800 ambao walitelekezwa na baba zao, sasa hivi wanawahudumia vizuri watoto wao, hivyo hawa watakaoanza kidato cha tano nitawasimamia", amesema Makonda.
Machi 8 kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine duniani katika kuazimisha siku ya wanawake Duniani, lengo likiwa ni kutambua mchango wa wanawake katika shughuli za maendeleo.