Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku tano kwa wakurugenzi wa manispaa za Ilala na Kinondoni kuhakikisha ujenzi wa miradi iliyotengewa fedha imeanza.
Makonda ameyasema hayo mapema leo alipokutana na Wakuu wa Wilaya na watendaji kujadili miradi ambayo haijafikia malengo.
Amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam ziko fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ikiwemo machinjio ya Vingunguti na uendelezwaji wa fukwe ya Coco ambapo pesa zilikwishatolewa na Rais Magufuli.
"Natoa siku tatu kwa mkurugenzi wa Ilala awe amesaini mkataba wa machinjio ya Vingunguti na mkurugenzi wa Kinondoni awe amesaini mkataba wa uendelezwaji wa Ufukwe wa Coco na ndani ya siku tano miradi hiyo iwe imeanza".
Makonda ameongeza kwamba Fedha zilishatolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Dar es salaam cha kushangaza hakuna mradi ulioanza,".