Mama mjamzito aliyetumia mtandao wa YouTube kujifungua afariki dunia, Polisi wadai aliogopa kutengwa

Mwanamke mmoja mjamzito mjini Gorakhpur nchini India, amefariki dunia chumbani kwake akijaribu kujifungua peke yake bila msaidizi, kwa kuangalia video kwenye mtandao wa Youtube namna ya kujifungua.


Taarifa iliyotolewa na Polisi juzi Jumatatu mjini Gorakhpur, imeeleza kuwa wapangaji wenzake ndio walikuwa wa kwanza kuona damu ikitoka chumbani kwake na kutoa taarifa polisi.

Polisi wamesema walimkuta marehemu amefariki, huku kichwa cha kichanga kikiwa kimekwama kwenye mlango wa kutokea.

Akiongea na gazeti la India Times jana Jumanne, Kamanda wa Polisi mjini humo, Ravi Rai amedai kuwa, walimkuta marehemu ameshika simu iliyokuwa ikionesha video za wanawake wakijifungua huku TV yake ikiwa na CD inayoonesha video za namna ya kujifungua.

Polisi walikuta mikasi, viwembe, panaldo na pamba vifaa vyote vikiwa vimetapakaa damu.

Baba mwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, wakati anatoa maelezo polisi amesema kuwa, siku nne zilizopita alimuuliza mwanamke huyo, kuhusu hatima yake kwani alikuwa amefikia mwezi wa kujifungua na alikuwa anaishi peke yake, alimjibu kuwa mama yake atakuja.

“Nilimuuliza, alinijibu kuwa mama yake atakuja kumsaidia kumpeleka Hospaitali. Nikaamuliza kuhusu mumewe aliniambia hajaolewa.“ameeleza mzee Indra.

Wapangaje wenzake, wanasema mwanamke huyo aliwambia kuwa hana mume na ujauzito wake alibakwa hivyo asingepata msaada haraka na alikuwa anaogopa kuchekwa na wenzake.

Nchini India ni aibu mwanamke kuzaa mtoto asiye na baba yake, wengi wanatengwa kwenye jamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad