Mama Yangu Hamtaki Mume Wangu Kwa Sababu Alikuwa Mtumishi Wetu


Aslam aleykum

Mimi niliolewa mara ya kwanza na binamu yangu, haikufika muda tukaachana, nikaja  kupata mchumba  ambae alikuwa ni mfanyakazi wa mama yangu, mama akakataa mimi niolewe na huyo mvulana,upande wa baba wakaniozesha, mama akaniambia nisiende nyumbani wala kwa ndugu yake yeyote, mimi nikawa nina kwenda lakini kila nikifika mama anatoka nyumbani,kwa kweli ilikuwa ikiniuma sana lakini nilikuwa sina jinsi sababu nilishaamua kuolewa na nampenda mume wangu na nampenda mama yangu,kwa kweli ilikuwa ni muda mgumu sana kwangu,ikafika muda, mama yangu akatuma maneno ya vitisho yani kama tusipoahana atamfanyia mume wangu kitu kibaya,mume wangu akawa na mawazo sana sababu yeye alikuwa si mzaliwa wa hapo,kwahiyo akaingiwa na hofu ikabidi tuachane,lakini tulipanga kuwa tutakuwa tunaonana pale kila mmoja atakomuhitaji mwenzake.

Akaniandikia talaka moja nikarudi nyumbani mama yangu alifurahi sana aliponiona,haikufika muda tukakutana kimwili mimi na mume wangu, tukawa kila siku za mapunziko tunaonana,lakini hatukai nyumba moja,lakini tuko mji mmoja, Baada ya mienzi mimi nikapata safari lakini kabla sijaondoka tukatafuta sehemu  tukakaa wiki nzima ili tuwe na muda wa kuongea kwa kina.

Sasa niko mbali na mume wangu lakini tunawasiliana kama kawaida je bado tunaishi kama mume na mke au? je nikirudi nirudi kwangu au niendelee kuishi na mama? na mama hataki hata kusikia ndugu na majamaa na marafiki wote wameongea nae lakini hamtaki mume wangu hata kumuona na sisi tunapendana.

Naombeni msaada wenu wa kiislam ndugu zangu kama Allaah (SW) alivyosema kuhusu ndoa basi naombeni misaidi kwa hili linalonisibu. 

 SHUKRANII.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad