MANCHESTER United inasemekana inafukuzia mastaa watatu ili kuimarisha kikosi chao cha msimu ujao.
Mastaa wanaotakiwa ni pamoja na beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, staa wa Napoli, Kalidou Koulibaly na kiungo wa Ivan Rakitic anayekipiga Barcelona.
Manchester United inaamini kuwa mastaa hao watatu watasaidia timu hiyo kwenda sawa na Liverpool na
Timu hiyo inataka kusuka kikosi cha kuweza kupigania mataji England na Ulaya kwenye msimu ujao.
Wan-Bissaka anang’ara kwenye Ligi Kuu England, ambapo ameichezea Palace mara 37 kwenye Ligi Kuu England tangu msimu uliopita.
Dogo huyo mwenye umri wa miaka 21 anatakiwa ili kurithi mikoba ya wakongwe Ashley Young na Antonio Valencia.
Mabeki wa pembeni Young na Valencia wote wana miaka 33, ambapo ina maana kuwa umri wao sasa unaanza kuwatupa mkono.
Koulibaly anatakiwa na Manchester United ili kusaidia kuimarisha safu ya ulinzi akiwa beki wa kati.
Rakitic ni kati ya mastaa wa dunia, ambapo sasa inaaminika kuwa anataka kuondoka Barcelona kutokana na hofu ya namba kufuatia klabu hiyo kumsajili mholanzi Frenkie de Jong.