Mashabiki wa Leicester City kunywa pombe za bure leo

Klabu ya Leicester City inatarajia kufanya ‘birthday’ ya aliyekuwa mmiliki wa timu hiyo, Vichai Srivaddhanaprabha kwa kuwapatia mashabiki wake pombe za bure pamoja na keki kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Bournemouth.

Beer & cakes: Leicester City fans to celebrate late owner's birthday at Bournemouth game
Makamu mwenyekiti klabu ya Leicester City, Khun Aiyawatt Srivaddhanaprabha ameamua kutoa ofa hiyo ya kuwapatia bia za bure, keki na maji mashabiki wote wa timu hiyo kwenye mechi yao ya leo siku ya Jumamosi.


Klabu hiyo ilitoa taarifa rasmi juu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Srivaddhanaprabha ambapo watakuwa pamoja na mashabiki huku kifo cha mmiliki huyo kilitokana na ajali ya ‘helicopter’ kwenye mechi dhidi ya West Ham iliyomalizika kwa sare ya 1 – 1 mwezi October.

“Kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Vichai Srivaddhanaprabha tutawashukuru mashabiki kwa sapoti yao katika kipindi chote cha huu msimu. Makamu mwenyekiti, Aiyawatt na familia ya Srivaddhanaprabha itatoa bia za bure, maji pamoja na keki kwa kila mtu atakaekuwa na tiketi ya mechi yetu ya leo.”Taarifa iliypotolewa na uongozi wa klabu hiyo.

Beer & cakes: Leicester City fans to celebrate late owner's birthday at Bournemouth game

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad