Mauaji ya Njombe: Waganga wa tiba za jadi wakamatwa kwa tuhuma za mauaji ya watoto

Mauaji ya Njombe: Waganga wa tiba za jadi wakamatwa kwa tuhuma za mauaji ya watoto
Polisi nchini Tanzania imewakamata waganga 65 wa tiba za jadi wanaoshukiwa kuhusika na mauji ya kikatili ya watoto kusini magharibi mwa taifa hilo.

Hii inafuatia mauaji ya watoto 10 katika maeneo ya Njombe na Simiyu mwishoni mwa Januari mwaka huu:

Mkuu wa polisi Simon Sirro amethibitisha kuwa waganga 45 wa tiba za jadi wamekamtwa katika eneo la Simiyu na wengine 20 katika eneo la Njombe.
'

"Kuna sababu nyingi ambazo huenda zilichangia mauaji hayo lakini wao wanatuhumiwa kutokana na kuhusika kwao na imani za kishirikina.'' alisema bwana Sirro.

Ameongeza kuwa washukiwa hao wanahojiwa kuhusiana na mauaji ya watoto yaliyosababisha mjadala wa kitaifaTanzania.


Mkuu huyo wa polisi aidha amesema kuwa msako mkali dhidi ya waganga hao ambao ni washukiwa wakuu wa mauaji hayo yamekuwa yakiendelea tangu wiki moja iliyopita.

'Nimetoa amri kuwa kila mganga wa tiba za jadi waliyosajiliwa na wale ambao hawajasajiliwa wachunguzwe na wale watakaoshukiwa kuwa wahalifu wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria''


Alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Polisi inawalenga wanaganga wa jadi ambao hawajasajiliwa rasmi kuendesha shughuli zao.

'Mapema mwaka huu watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 katika maeneo ya Njombe na Simiyu walipatikana wamefariki katika mazingira ya kutatanisha.

Serikali ya Tanzania iliahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji hayo ya kikatili.

Watu waliyo na ulemavu wa ngozi ni miongoni wahasiri wa mauji yanayohusishwa na imani za kishirikina ambapo sehemu za miili yao hutumiwa kufanyia matambiko

Waganga wa tiba za jadi wilayani Njombe hata hivyo wamejitenga na tuhuma kuwa wanachochea mauaji ya watoto wilayani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad