Maumivu Wakati wa Kufanya Mapenzi Kwa Mwanamke
0
March 07, 2019
Maumivu wakati wa kufanya mapenzi ni hali inayojitokeza hasa kwa wanawake. Hujulikana kwa kitaalamu kama.
dyspareunia. Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa kufanya mapenzi au baada ya kufanya mapenzi. Sababu kuu za maumivu haya mara nyingi ni magonjwa ya zinaa na kupungua kwa majimaji ukeni wakati wa ngono.
Maumivu Wakati Wa Kufanya Mapenzi
Unaweza kuwa unapata maumivu wakati tendo la ngono linaendelea. Mara nyingi maumivu haya huwa kwenye kuta za uke, shingo ya uzazi au chini ya kitovu. Sababu za maumivu haya ni;
Kuchubuka ukeni kutokana na maji ya uke kupungua. Inawezekana kutokana na kutoandaliwa vizuri wakati wa mapenzi au uke kutotoa majimaji ya kutosha.
Magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, vaginitis.
Maambukizi ya shingo ya uzazi (cervicitis)
Maambukizi kwenye mirija ya uzazi. Mara nyingi amumivu hutokea chini ya kitovu au kiuononi.
Maumivu Baada ya Kufanya Mapenzi
Baada ya kukutana na mwenzi wako kingono, unaweza kuanza kupata maumivu dakika chache mpaka siku kadhaa toka mlipokutana. Maumivu ya kawaida huwa ni kwenye uke kutokana na kuchubuka wakati wa kufanya mapenzi. Unaweza kuyahisi vizuri hasa pale unapojisafisha kwa maji au wakati wa kukojoa ikiwa njia ya mkojo imechubuliwa.
Maumivu ndani ya uke kabisa, kiunoni au chini ya kitovu baada ya kufanya mapenzi mara nyingi huonesha dalili za
Maambukizi ya shingo ya uzazi
Maambukizi ya mirija ya uzazi
Saratani ya shingo ya kizazi
Dalili hii inaweza kuambatana na hali ya homa, kutokwa damu ukeni baada ya ngono, kutoa uchafu ukeni, kutapika na kichefuchefu.
Matibabu
Unapopata hali hii jichunguze vizuri. Kama maumivu hayajatokana na michubuko wakati wa mapenzi, basi onana na daktari haraka iwezekanavyo. Maambukizi ya shingo ya uzazi na mirija ya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease – PID) huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii. Matibabu ya haraka ni muhimu ili kupunguza madhara ya magonjwa haya.
Michubuko kutokana na kufanya mapenzi hupona yenyewe polepole. Jioshe vizuri kwa maji safi. Usipake dawa zozote mpaka uambiwe na daktari wako.
Tags