Mchezaji wa YANGA Makambo azidi kung’ara


Mshambuliaji wa Yanga SC, Mkongoman Heritier Makambo amezidi kung’ara baada ya kuchaguliwa kwenye orodha ya awali ya Wachezaji 40 watakaounda kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo.

Congo ni kati ya timu zinazochuana kuwania kufuzu mashindano ya kimataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika nchini Cameroon.

Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera alisema mshambuliaji huyo yumo kwenye mchujo wa wachezaji 40 watakaounda kikosi cha Wachezaji 23 watakaoichezea DR Congo.

Zahera alisema mshambuliaji huyo ameitwa katika kikosi hicho cha awali kutokana na kiwango kikubwa ambacho amekionyesha akiwa na Yanga tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi.

“Congo tuna utaratibu wetu wa kuita wachezaji wa timu ya taifa ambao siku 15 kabla ya kutangaza timu itakayoiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali, tunatangaza wachezaji 40 wa awali na baada ya hapo kufanya mchujo na kufikia 23.

“Wachezaji hao 23 ndiyo watakaounda timu ya taifa na kikubwa tunachokiangalia ni kiwango cha mchezaji kutokana na nafasi anayoicheza katika klabu yake", alisema Zahera

Pia amesema kuwa kikubwa Kikubwa anachotakiwa kukifanya hivi sasa Makambo ni kuendelea na kasi yake ya kufunga mabao ili kufanikisha malengo yake aliyojiwekea ya Siku moja kuichezea timu ya taifa ambayo tayari imeanza kutimia.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad