Mdau Kamfungukia Diamond "Kwa kuwa wewe DIAMOND Hubanduki Wala Hupindui kwa Mama yako, Watoto Wako Pia Watafanya Hivyo Hivyo Kwa Mama zao"
0
March 05, 2019
Barua ya wazi Kutoka kwa Mdau Kwenda Kwa Diamond:
Diamond Platnumz natamani huu ujumbe ukufikie haraka iwezekanavyo. Perhaps tayari unalijua hili kama hujui soma kwa makini.
Mimi sio mwanasaikolojia wa watoto wala wakubwa au wazee, lakini najua mawili matatu ambayo naruhusu kukosolewa.
Watoto wako sasa hivi hawako na wewe, wote wako kwa mama zao. Na wewe uko na mama yako. Hiyo siyo coincidence. Sasa hivi watoto wako wanaishi maisha uliyoishi wewe utotoni na itakuwa hivyo milele unless uamue kubadili mambo.
Yawezekana mzee wako alikunyima kuwa nawe alipowaacha na mama, na sasa huna sababu ya kumtafuta, fine. But trust me maumivu anayoyapata huyu mzee na wewe lazima utayapata ukifika umri wake usipofanya kitu katika kipindi hiki.
Akina Nilan na Dylan hawatakuja kukujali wala kusumbuka kukutafuta si kwa sababu watakuwa nanakuchukia, no. Tena watakuwa wanakupenda na kukukumbuka kwa mengi lakini hawatakutafuta. Sababu itakuwa ni jinsi walivyokuona huna time na mzee wakajifunza kutoka kwako kuwa baba hana umuhimu wa kutafutwa. History will start to repeat itself.
Pesa na matunzo unayotuma kwa wazazi wao hazitawafanya wakujali, hapo unawafundisha kuwa na wao wakipata watoto wao watoe pesa za kuwatunza pia. Which is excellent. Lakini...
Kwa kuwa wewe hubanduki wala hupindui kwa mama na wao hawatapindua wala kubanduka kwa mama zao. Kwa kuwa wewe unamspoil mama Sandra na wao wakipata utajiri kama wewe watawaspoil mama zao wakuache wewe kama mzee Abdul. Hasa watoto wa kiume Sababu wewe ndio role model wao numero uno. Itawachukua nguvu kubwa sana kujifunza otherwise.
Kuamua kuwatembelea mara kwa mara au kuwachukua uishi nao haitabadili chochote, hiyo itawafanya tu nao wawachukue watoto wao waishi nao pia, lakini si kuishi na wewe uzeeni.
Ushahuri wangu kwako,
Kama unataka hawa madogo waje wakupende ukubwani mwao wewe ukiwa mzee hakikisha wanakuona jinsi unavyomjali mzee Abdul, hata kwa kujilazimisha.
Children learn by examplary actions.
LIKE FATHER LIKE SON.
By Mwaugulumu Mwamengele