Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee amesema kwamba hakutoa neno lolote baada ya Lowassa kurudi kwenye Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa anatambua changamoto anazozipitia kiongozi huyo kwa sasa.
Mdee amefunguka hayo wakati akijibu swali kuhusu maoni yake kufuatia aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mgombea huyo wa Urais mwaka 2015 kwa mwamvuli wa Ukawa, tangu aliposema 'amerudi nyumbani'.
"Natambua changamoto nyingi anazopitia za kifamilia na kibiashara, akalazimika kuomba po! sikuona haja ya kusema chochote nikiheshimu uamuzi wake. Najua nafsi yake inavuja damu ya usaliti kwa waliompa heshima na ‘kumrudishia uhai’"Halima James Mdee.
Edward Lowassa alirejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, ya wiki iliyopita na kupokelewa na uongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti, Dk. Joh Pombe Magufuli.
Baada ya kurejea CCM, Lowassa hakuzungumza chochote zaidi ya kusema tu kuwa, "nimerudi nyumbani".