Mgomo wa Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta umesababisha abiria kukwama kusafiri mjini Nairobi
Wafanyakazi wa usafiri wa ndege wameanza mgomo kupinga mpango wa kuunganishwa shughuli za usimamizi vya uwanja huo wa ndege kati ya shirika kuu la ndege nchini Kenya Airways na mamlaka ya usimamizi wa viwanja wa ndege KAA.
Muungano wa wafanyakazi hao (KAWU) umeuliza maswali kuhusu mipango hiyo ya kuunganisha shughuli kati ya pande hizo mbili na sasa unaitisha mageuzi katika usimamizi wa Kenya Airways na shirika la usimamizi wa viwanja vya ndege KAA.
Sambamba na hilo wafanyakazi wanatuhumu na kupinga makosa yanayofanyika katika uajiri wa wafanyakazi.