MIMBA aliyonayo staa wa filamu za Kibongo, Ester Kiama ilitaka kumtoa roho baada ya kumsababishia kuumwa takribani miezi miwili bila kuinuka kitandani ambapo anadai alihisi kuchungulia kaburi kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda Ester alifunguka kuwa aliumwa sana mpaka akawa anaogopa hata kujionyesha kwa watu kutokana na alivyokonda kwani ujauzito alionao ulimsababishia kuwa na hali mbaya ingawa kwa sasa anamshukuru Mungu anaendelea vizuri.
“Jamani nilichungulia kaburi kabisa, niliumwa sana lakini nafikiri ni kipindi tu cha mpito na niseme tu namshukuru Mungu kwa kunijaalia zawadi hii na ninamuomba sana anikamilishie safari yangu nimalize salama” alisema Ester Kiama.