Mkurugenzi wa Takukuru Aliyetajwa na Rais Magufuli kwa Kuwadhurumu Viwanja Wafanyakazi Wenzake Atiwa Mbaroni

Mkurugenzi wa Takukuru Aliyetajwa na Rais Magufuli kwa Kuwadhurumu Viwanja Wafanyakazi Wenzake Atiwa Mbaroni
Mkurugenzi wa Mipango TAKUKURU, Kulthum Mansoor, ambaye Machi 28, 2019, alitajwa na Rais Magufuli kwa tuhuma za kuwadhulumu viwanja, baadhi ya wafanyakazi wenzake wa TAKUKURU amekamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Oysterbay.

Kulthum amekamatwa jana Alhamisi Machi 28, 2019 na kupelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa  kwamba wakati jana Rais  Magufuli alipokuwa anamzungumzia kigogo huyo, uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ulikuwa umekamilika

Jana, Rais Magufuli akizungumza Ikulu mara baada ya kumuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola alisema anashangazwa kwa taasisi hiyo kutomchukulia hatua yeyote Mkurugenzi huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad