Imeelezwa kuwa wawili hao walikamatwa juzi na kupelekwa mahabusu kituo cha polisi cha Bomang’ombe wilayani Hai na kwamba fedha hizo inadaiwa alipewa dereva wake huyo ili ampelekee ofisini.
‘Ni kweli nimeagiza huyo dereva akamatwe ili uchunguzi ufanyike kujua ni kwa nini apewe Sh1 milioni ili aniletee ofisini ili nikatembelee kiwanda cha (jina limehifadhiwa). Hili ni kosa,‘amesema Ole Sabaya na kuelezea majukumu yake kiama kiongozi.
‘Mimi nadhani ni makosa, kwani mimi kama kiongozi wa Serikali ni wajibu wangu kutembelea viwanda na maeneo mengine yanayotoa huduma kwa jamii,’.
Tayari watuhunmiwa hao wawili, wameanza kuhojiwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani humo.
DC Ole Sabaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo alisema baada ya kupelekewa fedha hizo ofisini aliagiza vyombo vya usalama kumkamata na kufuatilia kiwanda hicho.
Kwa upande mwingine, Sabaya pia ameagiza Takukuru kufuatilia kiwanda hicho na ofisa aliyetoa fedha ili kujua lengo lao lilikuwa ni nini