Mtandao wa Instagram waja na huduma ya ‘Instagram Shopping’,

Mtandao wa Instagram waja na huduma ya ‘Instagram Shopping’,
Mtandao wa kijamii wa Instagram unaendelea kufanya maboresho kila kukicha, na awamu hii umekuja na Instagram Shopping, Ambapo wanunuaji watanunua bidhaa na kulipia moja moja kupitia mtandao huo huo.


Ili kuweza kulipia utahitaji uwe na akaunti ya benki pekee yenye huduma ya Visa, Mastercard au akaunti ya Paypal.

Kwa sasa ukihitaji bidhaa hutaingia tena kwenye website za manunuzi kama (Amazon na Alibaba) na badala yake utalipia moja moja kwenye akaunti yako ya Instagram.

Kwa mfano, kama unataka kutoka kampuni ya Adidas, utaingia kwenye ukurasa wa Instagram wa Adidas na kisha kuchagua kiatu unachohitaji.

Ukimaliza utabofya picha ya bidhaa husika litatokea neno lililoandika “TAP TO VIEW PRODUCT” na kisha litakuja jina la bidhaa na gharama yake ukibofya hapo, utakutana na maelezo zaidi ya kulipia ambapo utajaza anwani yako, majina yako, barua pepe na namba za simu kisha utalipia kwa njia ya mtandao, yote hayo utafanya ukiwa ndani ya Instagram.


Ujio wa huduma hii, huenda likawa pigo kwa mitandao maarufu inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa mitandao kama Amazon na Alibaba, kwani kwa sasa Instagram ndio mtandao unaokuwa kwa kasi zaidi duniani.

Huduma hii ya ‘Instagram Shopping’ imezinduliwa jana na kama bado huipati kwenye akaunti yako fanya updates ya App yako

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad