Mtoto wa Aliyekuwa Rais wa Liberia Ashtakiwa kwa Kosa la Uhujumu Uchumi

Mtoto wa Aliyekuwa Rais wa Liberia Ashtakiwa kwa Kosa la Uhujumu Uchumi
Mtoto wa aliyekua rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ameshtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi uliohusisha vitendo vya uchapishaji wa fedha cha mamilioni ya dola kinyume cha sheria.

Charles Sirleaf anashukiwa kufanya vitendo hivyo alipokua Gavana wa Benki kuu mwaka 2016-2018.

Maafisa wengine wa zamani wanne wa Benki wameshtakiwa pia.

Watuhumiwa mpaka sasa hawajesema lolote kushusu shutuma dhidi yao.

Ripoti kuhusu mamilioni ya fedha yaliyopotea ilitolewa juma lililopita.

Moja kati ya nchi masikini sana, Liberia imekua ikijinasua kwenye vitendo vya rushwa vilivyokithiri.

Ellen Johnson Sirleaf,raisa wa taifa hilo tangu mwaka 2006 mpaka 2018, alisifika kwa kuuinua uchumi baada ya miaka kadhaa ya mzozo nchini humo.

Siku ya Jumatatu, Bwana Sirleaf, Mkuu wa zamani wa benki Milton weeks na afisa mwingine wa benki,Dorbor Hagba wameshtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya fedha za Umma na kupanga njama za uhalifu.

Jaji wa mjini Monrovia, aliamuru wawekwe gerezani wakisubiri kusomewa mashtaka.

Wanasheria wa watuhumiwa hawajazungumza lolote kuhusu shutuma dhidi ya wateja wao.

Ripoti hiyo imegundua nini?
Ripoti hiyo iliandikwa na taasisi iliyofanya uchunguzi iitwayo firm Kroll.

Ilikua ikitazama mazingira ya kupotea kwa dola milioni 100 za marekani zilizokuwa zimechapwa mwaka jana.

Iliripotiwa kuwa makontena yaliyokua yamejaa noti yalitoweka kutoka bandari ya Monrovia na uwanja wa ndege.

Hata hivyo, Ripoti hiyo haikua na ushahidi wa kutokea vitendo hivyo.

badala yake, iliaini kuwa benki kuu ya Liberia ilishirikiana kinyue cha sheria kuchapa noti na kuziingiza nchini mara tatu zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa kuchapwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad