Muna Love Aamua Kujilipua Awachana Wanawake Wanaochukua Waume za watu

Muigizaji, Muna Love ametoa ujumbe kwa wanawake wenye tabia za kuchukua waume za watu na kuwategea kuzaa nao.

Muna ametumia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa jambo wanalolifanya wanawake wa aina hiyo wanaowatoa machozi wanawake wenzao watalipwa tu siku isiyo na jina.

Muna amesema kuwa anajua kuwa watu wenye matukio kama hayo watamchamba ila ukweli anatoa kwasababu hata yeye alikuwa hivyo, huku akisema kuwa anachokiandika hata yeye alikiishi.

"Leo ninaujumbe kwa wanawake, wale wenye tabia za kuchukua waume za watu, kuwategea kuzaa nao, kuwateka zaidi wanaume na kuwasahaulisha familia zao. Jambo mnalotakiwa kujua Yoote mnayoyafanya sasa mkijiona wajanja eti mnaenda na wakati kumtoa machozi mwanamke mwenzenu mtalipa tu iko siku isiyokuwa na jina. Yaani kwa njia yoyote ile niamini mimi kila chozi mlilosababisha mtalilipa au vizazi vyenu vitadaiwa."

"Nikusihi sana ewe mwanamke ambae leo mmeo hatulii nyumbani, amekua ni shubiri nyumbani Futa chozi sasa na umshukuru Mungu, Angalia ni kipi ambacho mmeo hakipati ili ukitimize maana adui hutumia udhaifu huo, Pia mshukuru Mungu kwa Hali Yote unayopitia na umtegemee yeye tu. Na utubu kwa dhambi unazozikumbuka na usizozikumbuka maana inaweza ikawa unalipa Adhabu ya wazazi wako, kwa sababu hujui au ulifanya mwenyewe ukasahauna, hiyo dhambi itaendelea kukutafuna mpaka mwisho," aliongeza.

"So ni lazima utengeneze kwanza mapito yako na Mungu wako, ukiri kumkosea na ukubali akufinyange upya na akutengeneze upya haijarishi njia atakayoitumia Kukunyoosha ila Zoote ni njema kwake."

"Najua wale wenye haya matukio mtachama ila ukweli natoa (Inakuja Part 2) maana hata mimi nilikua hivyo. Ninachoandika na mimi nilikiishi," ameandika kwa msisitizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad