Mwenyekiti Kiboko Aishauri Serikali Kuhalalisha Uchangudoa ili Kujipatia Mapato

Mwenyekiti Kiboko Aishauri Serikali Kuhalalisha Uchangudoa ili Kujipatia Mapato
Mwenyekitwa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Simon Tyosela ameishauri serikali kuhalalisha biashara ya akina dada wanaoujiuza, maarufu machangudoa.

Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua ukusanyaji mapato ya halmashauri mbalimbali nchini.

Alitoa ushauri huo, kutokana na kauli ya Mkuu wa Mkoa, Dk Rehema Nchimbi kueleza kuwa madada poa na machangudoa wote mjini hapo kukamatwa.

Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati wa Kikao Maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichopitia na kupitisha Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

Tyosela amesema kutokana na halmashauri nyingi nchini kukwama kukusanya mapato, ingekuwa jambo jema kama serikali ingehalalisha biashara ya machangudoa kama zilivyo biashara nyingine.

"Niseme sikubaliani kamwe na suala la ushoga. Lakini hili la machangudoa nashauri lirasimishwe ili serikali iweze kujipatia mapato,"alisema na kuongeza "Iwapo watashindwa kulipa kodi hiyo, basi watakuwa wamejiondoa kwa hiyari yao wenyewe kwenye biashara hiyo, badala ya utaratibu uliopo wa polisi kuwakamata."

Meya wa Manispaa ya Singida, Gwae Mbua alipinga ushauri huo, kwa madai kuwa hatua hiyo itadhalilisha taifa.

"Wanaojiuza ni ndugu zetu, dada zetu na watoto wetu... wamekuwa wakitutia aibu. Sikubaliani na wazo la Mwenyekiti wa Iramba kuhalalisha biashara hiyo kwa kuwa ni kinyume na utamaduni wa Mtanzania,alisema.

Aliongeza "Naomba wabunge waliopo humu wajifanye kama vile hawajasikia ushauri wa ndugu yangu huyu. Kuna namna nyingi za halmashauri kujipatia mapato, kinachotakiwa ni watendaji wetu kuwa wabunifu zaidi katika kubuni vyanzo vipya halali vya mapato na sio hii ya kuuza miili."

Awali, kwenye kikao hicho cha RCC, Mkuu wa Mkoa, Dk Nchimbi alisema hakuna taifa linaloweza kuwa nchi ya viwanda na kuingia kwenye uchumi wa kati kwa kuendekeza vitendo vya kipuuzi kama vile akina dada kujiuza miili yao.

Alisema kuwa katika kuhakikisha mkoa unakuwa tulivu na unashughulika zaidi na maendeleo ya wananchi, umejipanga ipasavyo kuwaondoa machangudoa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad