Mwigulu Amjia Juu Zitto Kabwe, Msaada Chanzo

Mwigulu Amjia Juu Zitto Kabwe, Msaada Chanzo
Mbunge wa Iramba Magharbi, Dk. Mwigulu Nchemba amemjia juu Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kwamba hajaona utu kwenye tendo la msaada uliotolewa na serikali ya Tanzania kwa nchi tatu Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kufuatia maafa ya kimbunga yaliyowakuta.

Mwigulu amefikia hatua hiyo baada ya Zitto kukosoa hatua ya baadhi ya wakereketwa na wafuasi wa CCM kuutangaza msaada huo huku akiweka maneno ya 'kwa hisani ya Watu wa Tanzania, jambo ambalo ameliita ni ushamba.

Dk. Mwigulu ameshangazwa na Kauli ya 'Kishamba' iliyotumiwa na Zitto ambapo amesema kauli hiyo inatumiwa na mtu anayelilia ustaarabu wakati yeye si mstaarabu, huku akihoji kwanini hajaona utu uliofanywa na badala yake ameona siasa.

"Kishamba Shamba na Kishetani?. Hii ni lugha ya mtu anayelilia ustaarabu pasipokuwa mstaarabu. Kwa utekelezaji mkubwa namna hii wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa jitihada za Rais?, hakuna kijiji hakijaguswa. Msaada ndio uwe wa kufanyia Siasa?", ameandika Dk. Mwigulu.

Ameongeza kuwa, "Usivyo na utu, huoni utu unaona siasa".


Katika kauli, Zitto alisema kwamba, "Wakati wa Uongozi wa Jakaya M Kikwete wenzetu Zimbabwe walipata maafa ya njaa tukawapelekea chakula tani zaidi ya 8,000 za Mahindi. Hapakuwa na tambo za kishamba shamba na kishetani namna hii. Unafanyia Siasa msaada kwa wenzetu wenye maafa?. Bila hata aibu?".

Serikali ya Tanzania ilitoa msaada wa tani 214 za chakula na dawa tani 24 (thamani zake hazikutajwa) kufuatia Kimbunga cha Idai nchini Malawi, Msumbiji na Zimbabwe ambacho kilikadiriwa kupoteza maisha ya watu takribani 1,000.

Jumanne Machi 19, 2019 Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu walikabidhi msaada huo kwa mabalozi wa nchi hizo nchini, kisha ikaanza kupakiwa katika ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuisafirisha.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Masada uliotolewa ulitolewa na watanzania, hivyo ni wajibu wa serikali kutujuza watanzania wote juu ya nini tumewafanyia ndugu zetu waliokumbwa na maafa kama nchi zote zifanyavyo. Serikali haikukosea kututaarifu. Binafsi nimefarijika mno kusikia Tanzania imerespond upesi sana. After all tunaishi katika zama za transparency kwani siri siri za matumizi ya resources zetu ndo mlango wa corruption. Well done serikali.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad