Mwili wa Ruge Kuwasili Mchana wa Leo na Kupelekwa Lugalo

Mwili wa Ruge Kuwasili Mchana wa Leo na Kupelekwa Lugalo
MWILI wa Mku­rugenzi wa Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, unatara­jiwa kuwasili nchini leo Ijumaa uki­tokea nchini Afrika Kusini.

Ruge alifariki dunia Jumanne jioni akiwa huko kwenye matibabu kwa muda na kwa sasa msiba upo nyumbani kwa baba yake, Miko­cheni jijini Dar.


Kwa mujibu wa Mse­maji wa Familia, Anick Kashasha, taratibu za kuaga mwili itakuwa ni Jumamosi.

Aliongeza kuwa Jumapili mwili huo utasafirishwa hadi Kizilu, Bukoba, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumatatu.

Watu mbalimbali jana walijitokeza kutoa pole kwa familia pale Mikocheni wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.

Pia wasanii wa Bongo Movie, Bongo Fleva na sanaa nyingine mbalimbali waliku­wepo kutoa pole kwa wafiwa na wengine walifanya hivyo kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake Majaliwa alisema: “Historia ya Ruge kwa upande wa serikali ni kubwa, kuanzia awamu ya nne na ya tano kwa kuwatu­mikia kikamilifu Watanzania kwa kuwasaidia vijana wengi kielimu na msaada wake wa hali na mali.

“Ruge alikuwa balozi wa kutafsiri Philosophy ya uzal­endo na fursa, vifo ni mpan­go wa Mungu tumuombee, salamu hizi ni kwa niaba ya serikali, kwa muda huu Rais John Magufuli anatimiza itifaki atakuja kutoa pole, tumuombee ndugu yetu.”

Naye Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema kuwa:

”Uthubutu na kujituma kwa Ruge ni darasa ambalo ameliacha kwa kila mmoja aliyekuwa akimfuatilia, ubunifu na juhudi ni alama itakayodumu.”

Kala Jeremiah ambaye ni msanii wa Bongo Fleva alisema: Kuondoka kwa Ruge kutabaki kwenye kumbuku­mbu kutokana na namna alivyokuwa akijitoa kwa ajili ya sanaa na kuwasimamia vijana.

“Nimefanya kazi na Ruge, alikuwa mshauri mzuri mfano ni mwaka 2015 ambapo alinishauri niyatoe mashairi ya Prof. Jay kwenye Wimbo wa Nchi ya Ahadi, aliona mbele kwa kuwa Profesor alikuwa ameingia kwenye siasa ninaamini atakumbukwa daima.”

Pia Shirikisho la Soka la Tanzania kupitia kwa Rais wake, Wallace Karia, jana walionyeshwa kuguswa na msiba huo pamoja na taa­sisi mbalimbali za Serikali. ambapo walituma salamu za rambirambi kwa wafiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad