Naibu Spika Atumia Dakika Tano Kukusanya Milioni Saba Za Ujenzi Wa Kanisa Makambako

Naibu Spika Atumia Dakika Tano Kukusanya Milioni Saba Za Ujenzi Wa Kanisa Makambako
Naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.TULIA ACKSON ameungana na wanawake wa kanisa la Tanzania assembles of God T.AG Makambako na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni saba zitakazo saidia ujenzi wa kanisa hilo.

Akiwa katika ibada ya maadhimisho ya sikukuu ya wanawake watumishi wa kristo wa kanisa hilo lililopo mjini Makambako,Dk Tulia kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge mkoani Njombe na wanawake wa kanisa hilo amesema kuwa wameshirikiana kukusanya fedha hiyo ili kuonyesha ushiriki wao katika Baraka ya ujenzi wa kanisa.

Hata hivyo Dk.Tulia amewakumbusha wanawake kuwalinda wanaume,kuilinda jamii ,Taifa pamoja na ulimwengu mzima kwa kuwa wanawake ndio tegemeo.

“Katika kitabu cha methali 31 kinazungumzia mama kufanya yampasayo kufanya,lakini kama wanawake tumepewa kazi ya kuwalinda wanaume na kwa maana hiyo tupaswa kuilinda jamii yetu,taifa letu na ulimwengu mzima unatutegemea sisi hasa wanawake wakrito wamchao bwana”Alisema Dk.Tulia

Makamu Askofu wa T.A.G  Njombe kaskazini ambaye pia ni mchungaji mwenyeji wa kanisa hilo Mch.PATRICK LUHWAGO amesema kuwa ili mwanamke aweze kufanikiwa katika utumishishi uliotukuka ana wajibu wa kujifunza kwa watu waliotangulia na waliofanya vizuri.

“Ili kufanya utumishi uliotukuka mwanamke anatakiwa kujifunza kwa waliotangulia na waliofanya vizuri kwa kuwa wapo waliofanya vibaya kama akina Sara waliokuwa wakimshauri mumewe awe na nyumba ndogo na ni mtumishi wake wa kazi na baadaye kuanza kugeuka na kuwa mkali ,kwa hiyo ushauri wangu kwenu muishi maisha matakatifu nay a kumpendeza Mungu”alisema Askofu PATRICK  LUHWAGO

Naye mbunge wa jimbo la Makambako DEO SANGA  ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kwa kuiwezesha halmashauri ya mji huo kupata fedha za miradi mbali mbali ukiwemo mradi wa ujenzi wa hospital.

JULIET MOLLEL na MONIKA MAZIKU ni miongoni mwa wanawake waumini wa kanisa hilo mjini Makambako wanasema kuwa kutokana na mafunzo waliyoyapata kama wanawake wataendelea kuwa walinzi na viongozi katika jamii.

“Kutokana na mafunzo haya hakika yametubariki na mh.Naibu spika ametukumbusha kitu kizuri sana kwamba mwanamke ni mlizi katika jamii yetu hivyo hatuwezi kuishia tu kuilinda jamii bali hata kuendelea kutoa elimu juu mafundisho ya neon la Mungu ili wanawake tuendelee kuwa na hofu ya Mungu”alisema MONIKA MAZIKU

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad