Nay wa Mitego amshushia ujumbe mzito Diamond ‘Ruge Ametutoa Mbali Natamani Ningemuona’

Nay wa Mitego amshushia ujumbe mzito Diamond ‘Ruge Ametutoa Mbali Natamani Ningemuona’
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka kuwa angefurahi kumuona msanii mwenzake, Diamond Platnumz akihudhuria mazishi ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba.

Akiongea na Bongo5, Nay wa Mitego amesema kuwa angefurahi kumuona Diamond anahudhuria kwenye msiba huo, kwani Ruge ni mtu ambaye wote wawili amewasaidia sana kuwakuza kwenye sanaa.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimefuatilia sana habari za Diamond na watu kumwambia amsamehe baba yake na pia ahudhurie mazishi ya Ruge. Kwanza kabisa lazima Diamond ajue kwamba actions talk better than words. Naona kila mara anajaribu kuonyesha kwamba yeye ni humble lakini je ni kweli ni humble rohoni? Mtu wa kawaida ambae ni humble hawezi kamwe kufanya anavyofanya Diamond. Tatizo kubwa naloliona kwake kwa sasa ni kiburi cha pesa. Kuna watu utawafanyia mema milioni lakini upungufu wako wa siku moja unawafanya wasahau mema yote uliyowafanyia. Hii si sahihi. Ukujiuliza kwa nini Diamond anamchukia mtu aliyemtoa katika umaskini unakosa jibu la maana. Hata kama Clouds walikuwa hawapigi nyimbo zake hapo mwishoni ajiulize ni kwa nini wakati nyimbo zake ndio zilikuwa zinapigwa miaka yote mpka akajulikana dunia nzima. kwa maana hiyo ina maana kuna mambo hawakuelewana na clouds kwa wakati huo. Na wala sio ajabu kwa watu wanaofanya biashara kufika mahali wasielewane. Yeye sio wa kwanza dunia nzima kufanyiwa hivyo. Hata wanamuziki maarufu duniani wanapitia mambo kama hayo. Kwa hiyo hiyo sio sababu nzuri ya kumchukia Ruge, mtu ambae amemtoa katika dimbwi la umaskini na kumfanya tajiri. Unapokuwa unapitia changamoto katika biashara ujue kwamba changamoto kama hizo zinataka kukufanya uwe na akili zaidi. Ukichukulia changamoto kwa jicho chanya ni lazima chamgamoto hiyo itakusaidia kupanda juu zaidi na sio kushuka chini. Tatizo letu wengi tunachukulia vitu juu juu tu bila kujua kwamba Mungu ana sababu na kila kitu. Sasa nikirudi kwa Diamond. Naloliona mimi kwake sasa linanitisha. Kuna methali inasema aliye juu mngoje chini. Nachokiona mimi kwa Diamond sasa hivi ni kwamba kiburi kimetangulia na anguko linafuata. Biblia inasema kiburi hutangulia anguko. Kitu kimoja ambacho mwanadamu napaswa kuelewa ni kwamba kusahau waliokufadhili wakati ulipokuwa na shida huleta laana kubwa sana kwenye maisha. Ogopa sana mtu aliyekuchukulia kama mdogo wake halafu akakufanya uwe ulivyo halafu ukamdharau na kumpiga kikumbo. Mungu huwa anasikia. Ogopa sana baba yako aliyekuleta duniani halafu akakuomba msamaha kwa kukukosea na akaomba umsaidie ukamdharau na kumwacha ataabike. biblia inatuonya tuwaheshimu baba na mama zetu ili tupate uhai mrefu. Haijasema tuwaheshimu wakiwa wazuri tu. Hata kama walitukosea ni wazazi wetu tunatakiwa kuwaheshimu na kuwajali. Diamond amekalia kaa la moto. Watanzania wameshajua kupitia kwa msiba huu wa Ruge na kwa kupitia malalmiko ya baba yake kwamba yeye ni mtu wa aina gani. Watanzania wameanza kujua pia kwamba Diamond waliomdhania sio sawa na Diamond wa kweli. Ushauri wangu kwa Diamond ni kwamba ameanza kushuka au kuchuja. Hana mvuto ule wa zamani. Kiburi kimemwingia na ameanza kuona kama pesa tu ndio za maana na wala sio binadamu. Hilo dio litakuwa anguko lake. Hakuna pesa yoyote inaweza kufanya yale binadamu wanaweza kufanya. Kama hatajinyenyekeza na kuendelea na kiburi basi ajue kwamba anguko linakuja. Bado ana nafasi ya kubadilisha mambo. Asijipe moyo kwa likes za instagram. Kuna watu wanalike tu hata hwajui wanalike nini. swali analotakiwa kujiuliza ni je, anaelekea juu au anaelekea chini? Jibu analo mwenyewe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Very good, interesting and teaching comment. Umesema yote nikiongezea nitaharibu. Mungu akubariki

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad