Ndege ya Kijeshi ya urusi yatua karibu na Caracas

Ndege ya Kijeshi ya urusi yatua karibu na Caracas
Ndege mbili za kijeshi za Urusi zilitua katika uwanja mkuu wa ndege wa Venezuela Jumamosi, zikiripotiwa kuwa na makumi kadhaa ya wanajeshi na kiwango kikubwa cha zana.

Ndege hizo zilitumwa "kutekeleza mkataba wa kijeshi wa kiufundi ", limeripoti shirika la habari la Urusi Sputnik limeripoti.

Javier Mayorca, mwandishi wa habari wa Venezuela, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba aliona wanajeshi wapatao 100 na tani 35 za vifaa vikishushwa kwenye ndege.

Trump 'hakusuka njama na Urusi' kushinda uchaguzi
Mwalimu wa Sayansi wa Kenya ashinda tuzo ya dunia
Taifa Stars yatinga AFCON baada ya miaka 39
Hii inakuja miezi mitatu baada ya nchi hizo mbili kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Urusi imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Venezuela, ikiikopesha nchi hiyo iliyoko Amerika Kusini mabilioni ya dola na kusaidia sekta yake ya mafuta na jeshi.

Urusi pia ilikuwa wazi kupinga hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo serikali ya rais wa Venezuelan Nicolás Maduro.

Bwana Mayorca alisema kwenye Twitter ndege ya kijeshi ya Urusi ya mizigo Antonov-124 na ndege ndogo aina ya Jet zilitua karibu na mji mkuu Caracas siku ya Jumamosi.

Alisema kuwa Generali wa Urusi Vasily Tonkoshkurov aliwaongoza wanajeshi hao walipokuwa wakitoka ndani ya ndege.

Ndege ya kijeshi ikiwa na nembo ya bendera ya Urusi inaonekana kwenye uwanja wa ndege Jumapili. Picha kwenye mitandao ya habari ya kijamiipia zilionyesha wanajeshi wamekusanyika katika uwanja wa ndege.

Mahusiano baina ya Moscow na Venezuela yameimarika katika miezi ya hivi karibuni , wakati uhusiano kati ya Marekani na Venezuela ukiwa mbaya zaidi. Mwezi Disemba, Urusi ilituma ndege za kijeshi aina ya Jet nchini Venezuela kama sehemu ya mazoezi ya kijeshi.

Mzozo wa kisiasa Venezuela wageuka mgogoro wa kimataifa
Urusi iliyalaani mataifa mengine ya kigeni kwa kumuunga mkono kiongozi wa upinzani wa Venezuela Juan Guaidó, ambaye alijitangaza kama rais wa mpito mwezi Januari.

Rais Maduro amemshutumu Bwana Guaidó kujaribu kupanga mapinduzi dhidi yake kwa usaidizi wa "Wavamizi wa Marekani".

Utawala wa Kremlin uliunga mkono kauli hiyo ,ukimshutumu Bwana Guaidó kwa "kujaribu kunyakua mamlaka kinyume cha sheria " akiungwa mkono na Marekani na ukaahidi kufanya "kila lipaswalo " kumuunga mkono Bwana Maduro.

Rais wa Urusi Vladimir Putin (Kulia) na mwenzake wa Venezuelan Nicolas Maduro ni washirika wa karibu
Bwana Maduro alipata ushindi kwa kura chache katika uchaguzi wa Aprili 2013 baada ya kifo cha aliyekuwa mshirika wake rais Hugo Chávez.

Alichaguliwa kwa muhula wa pili Mei 2018 katika uchaguzi ambao ulikosolewa sana na wakaguzi wa kimataifa.

Venezuela imekumbwa na mporomoko wa uchumi , huku uhaba wa chakula na mfumuko wa bei ukiongezeka na ukifikia walau kiwango cha 800,000% mwaka jana.

Bwana Guaidó amemtuhuma rais Maduro kuwa mtu asiyefaa kuwa rais, na alipata uungaji mkono wa wengi nchini humo pamoja na viongozi wa Marekani na Muungano wa Ulaya .

Serikali ya Maduro inaendelea kutengwa huku nchi nyingi zikiilaumu kwa mzozo wa kiuchumi, ambao umewafanya raia zaidi ya milioni tatu kuihama Venezuela.

Wakati huohuo, serikali ya Moscow imepanua ushirikiano na serikali ya Caracas katika miaka ya hivi karibuni - ikiongeza mauzo ya silahana kuongeza zaidi mikopo kwa nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad