Polisi wakamata waganga 16 Mwanza


Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kuwakamata Waganga wa jadi 16 wanaopiga ramli chonganishi kwenye jamii.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Muliro Jumanne Muliro amesema waliokamatwa ni wanaume 6 wanawake 10 wakiwa pamoja na nyara za serikali.

Amezitaja nyara hizo ni pamoja na mikia ya Nyumbu 2,magamba ya chatu, vipande vya mayai ya mbuni, pembe za Wanyama Pori nne, mafuta yanayodhaniwa kuwa ya Simba, ngozi ya Nyegere, vipande vinne vya ngozi vya wanyama pori aina mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad