Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ameamuru kuachiwa huru kwa mahabusu wanawake wote waliokamatwa kwenye maandamano ya hivi karibuni ya kumpinga kiongozi huyo.
Mapema mwaka huu Al-Bashir alitangaza hali ya hatari nchini humo na kufutilia mbali utawala wa majimbo na uongozi wake kufuatia kuibuka kwa maandamano.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Katika hotuba yake kwa taifa rais Bashir alisema kuwa maandamano yanayoshuhudiwa nchini yanalenga kuvuruga amani na kuhujumu utawala wake.
“Natangaza hali ya hatari kote nchini kwa mwaka mmoja.”
“Natangaza kuvunjiliwa mbali kwa utawala wa majimbo katika ngazi zote hadi za mikoa.”
Waandamanaji walimiminika katika mji wa Omdurman baada ya tangazo hilo, lakini waliyoshuhudia wanasema maandamano hayo yalizimwa na polisi kwa kutumia mabomu ya machozi.
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir atoa msamaha kwa mahabusu wanawake kwenye siku ya wanawake duniani
0
March 09, 2019
Tags