RC Ayoub amewaagiza Askari kushughulikia usalama wa Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja amewaagiza Askari wa Usalama barabarani kushughulikia usalama wa Wananchi katika matumizi ya barabara.

Amesema askari wa usalama wao ndio wenye jukumu la kushughulikia ipasavyo matumizi ya barabara.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha pamoja na viongzi wa wilaya zote Unguja, Wawakilishi na Wabunge katika utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi 2018/2019.

Ayoub amesema suala la matumizi ya barabara haiko salama miundo mbinu yake hairidhishi hata kidogo na inahatarisha usalama wa raia wakiwemo watu wazima ,walemavu, wagonjwa  na hata watoto wadogo.

Pia amesema hali  hatarishi zaidi iko kwa wanaoendesha daladala  kwani wao hawatendei haki abiria kwa kuwa wengi hawawafikishi vituoni mwao, pia wanafunzi wa skuli wanawanyanyasa  kwa kutowachukua  na wakiwachukua maneno ya bughudha hadi wanapofika vituoni mwao.

“Wanaoendesha dala dala ndio chanzo kikubwa cha kuhatarisha usalama wa raia kwa kufanya wanavyotaka ikiwemo kutokuwafanyia haki abiria kwa kuwapeleka wanapotaka kushuka , kuwanyanyasa wanafunzi  na pia boda boda hawafati sheria “, alisema Mwenyekiti huyo.

Hivyo amewaomba askari hao kuweza kushughulikia masuala haya ili wananchi waepukane na usumbufu wanaoupata  na kuhakikisha usalama wao wa safari unakuwa mzuri kwani Serikali inawajali wananchi wake na ndio  utekelezaji wa ilani wa Chama Cha Mapinduzi kutaka raia wawe salama .

Nae Naibu Waziri wa  Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mohamed Ahmada Salum amekiri suala hilo lipo na ameahidi kulisimamia na   kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na usalama katika matumizi ya barabara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad