Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemshauri, Mchungaji wa Daudi Mashimo, kuwapatia unabii familia ya aliyekuwa Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde na siyo kutangaza habari zake kwa vyombo vya habari.
Makonda ametoa ushauri huo kwa Mch. Mashimo baada ya kusambaa kwa video zikimuonyesha akidai kwamba aliyekuwa mtangazaji wa Jahazi Kibonde hajafariki na kwamba huenda familia yake imezika gogo au mgomba.
Katika mahuburi hayo ya Mch. Mashimo amesema kwamba Kibonde hajafariki kama ambavyo inaaminika, na kwamba hajafariki kwa mpango wa Mungu na yeye alipata maono hayo kabla ya kifo kutokea, "niiona na nikatangaza haya ni maono yangu ya kweli".
Makonda amesema kwamba hajawahi kuona kwenye biblia kwamba Manabii wa zamani walikwenda kwenye vyombo vya habari na badala yake walikwenda kwa wahusika.
"Ndugu yangu igependeza sana unabii huu ukawapatia wanafamilia na wala siyo kukimbilia kwa waandishi wa habari. Najaribu kupitia maandiko hapa bado sijaona Nabii alieenda kwa wanahabari badala ya kwenda kwa wahusika inawezekana labda Biblia yangu ni ya zamani", ameongeza Makonda.
RC Makonda Amuonya Mchungaji Mashimbo Kuhusiana na Kauli Aliyotoa juu ya Kifo Cha Kibonde
0
March 11, 2019
Tags