RC Makonda Atoa Agizo kwa Viongozi Wilaya za Dar es Salaam

RC Makonda atoa agizo kwa viongozi wilaya za Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  ameagiza viongozi wa wilaya za Dar es Salaam kuhakikisha mikataba ya miradi ya kimkakati inasainiwa na ujenzi uanze haraka iwezekanavyo.

Makonda amehoji sababu za fedha kuachwa benki bila kazi kufanyika. Ilala kuna mradi wa machinjio ya Vingunguti na Kinondoni mradi wa fukwe ya Coco.

Aidha Makonda amewaonya wakuu wa Idara zote wanaosimamia Miradi ya Kimkakati kuhakikisha inamalizika katika muda uliopangwa lakini pia wanazingatia viwango Kinyume chake wajiondoe wenyewe katika nafasi zao.

Miezi michache iliyopita Rais John Pombe Magufuri akiwa katika Uzinduzi wa ujenzi wa barabara za njia nane katika eneo la kimara jijini Dar es Salaam alishangazwa na baadhi ya Manispaa kushindwa kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo serikali ilishatoa fedha muda mrefu kwa ajili ya Utekelezaji wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad