Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amesema kuwa, Louis van Gaal ndiyo kocha bora kwa mbinu za ndani ya uwanja kuliko mwingine yoyote aliyewahi kufanya naye kazi katika ulimwengu wasoka hii ikiwa ni zaidi ya Sir Alex Ferguson.
Wayne Rooney has claimed that Louis van Gaal was 'tactically the best' he's worked with
Rooney ambaye anaongoza kwa idadi ya magoli ndani ya Manchester United kuliko mchezaji yoyote aliyewahi kuitumikia klabu hiyo amemwagia sifa kocha huyo raia wa Uholanzi aliyewahi kufanya naye kazi kwa miaka miwili na kuonyesha kushangazwa na kuteuliwa kwa David Moyes kurithi nafasi ya Ferguson mwaka 2013.
Rooney's claims come despite playing a large portion of his career under Sir Alex Ferguson
Nyota huyo amemuweka katika nafasi za juu, Van Gaal kama ndiye kocha bora zaidi katika mbinu aliyewahi kufanya naye kazi huku akimuacha legendari wa United, Ferguson pamoja na Moyes, Jose Mourinho.
Rooney admitted that David Moyes' appointment was a 'surprise' after Ferguson retired
”Nafikiri, David Moyes ila inashangaza kiasi kumchagua, lakini rekodi yake ya miaka 10 ndani ya klabu ya Everton ilikuwa nzuri,” Rooney amekiambia chombo cha talkSPORT.
”Mambo ya kimbinu hayakufanya kazi kwa Moyes akiwa Manchester United lakini Louis van Gaal alifanikiwa.
”Kwa mbinu yeye ni bora kuliko wote niliwahi kufanya nao kazi, kwenye mipango na kuweka sawa kwenye kujilinda kila moja anafahamu hizo sheria zake.”
”Ilikuwa katika mambo ya ushambuliaji sambamba na kujilinda alikuwa yupo vizuri.”
”Licha kuwa ameshinda makombe machache lakini hakuwa mbali na matumaini ya watu.”
Ferguson amesimamia jumla ya michezo 1,226 akiwa kama kocha wa United katika miaka yake yote 26 aliyokuwa klabuni hapo huku akifanikiwa kushinda jumla ya mataji 38 kwa Mashetani hao wekundu.
Van Gaal akiwa amesimamia michezo 103 akiwa United kwa miaka miwili, na kushinda taji la FA Cup akiwa na asilimia 52 ya kushinda kwenye mechi zake.