Rufaa ya Mbowe, Matiko kuunguruma tena leo

Kesi ya Mbowe na Matiko kuunguruma tena leo Mahakama Kuu
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo March 6, 2019 imepanga kusikiliza rufani ya kutenguliwa dhamana ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, na Mbunge Esther Matiko baada ya Mahakama ya Rufani kuagiza hivyo.

Utakumbuka March Mosi mwaka huu, Mbowe na Matiko walishinda rufaa ya dhamana yao dhidi DPP katika Mahakama ya Rufani.

Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Wawili hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad