Ruge Amefanya Mapinduzi ya Uendeshaji Vipindi vya Michezo Tanzania


Katika kipindi hiki cha maombolezo ya kuondokewa na Boss Ruge, vipindi vingi bado vya Clouds FM na Clouds TV vinazungumzia mambo mbalimbali kuhusu Ruge na watangazaji pia wanaeleza namna wanavyomkumbuka.

Jana Jumatatu March 4, 2019 siku ambayo Boss alipumzishwa kwenye nyumba ya milele, saa 3 usiku kama kawaida nilikuwa nasikiliza Sports Xtra hapo ndipo nilimsikia Alex Lwambano akielezea namna ambavyo Ruge alileta mapinduzi kwenye uendeshaji/utangazaji wa vipindi vya michezo Tanzania.

Vipindi vya michezo (vya radio) kwa miaka ya 1990 hadi 2000 mwanzoni, vingi vilikuwa vinafanyika kwa dakika 15 halafu kwa mfumo wa kutiririka (kusoma script mwanzo mwisho) zinapisomwa habari za kitafa na baadaye kimataifa.

Ruge alivyokuja akasema: “Nimefatilia kipindi chenu nanradio nyingine, badala ya kutangaza michezo hamuwezi kuzungumza/kujadili michezo?

Tukamuuliza kuzungumza ukiwa unamaanisha nini? Kwa sababu unajua kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine huwa kuna hali ya kusita kidogo.

Akasema: “Badala ya kuniambia Yanga imeifunga Pan Afrika 2-0 wafungaji ni fulani na fulani dakika za magoli na mechi imechezwa uwanja wa taifa sijui katolewa huyu kaingia yule mara kadi nyekundu…naona kwangu hainitoshelezi, hebu tutafute namna ya kwenda mbali zaidi.”

Sasa tukawa tunajiuliza, tunakwenda mbali kivipi? Akatuambia tutafute wataalam ili wawe wana-analyze lakini alikuwa anataka sisi tuzungumze zaidi kwa sababu kabla ya hapo kipindi kilikuwa kinaweza kufanywa na mtu mmoja anasoma script anacheza insert maisha yanaenda.

Sasa ikabidi tuanze kufanya kipindi watu wawili au watatu tunazungumzia mechi inayotarajiwa kuchezwa au iliyochezwa, hapo akasema hiki ndio nachotaka mimi.

Wakati huo tunafanya mabadiliko na akina Shaffih ndio wanaingia kwenye mifumo. Sasa unapotaka kuchambua inabidi uwe na kitu cha ziada hapo ndipo tukaanza kujiongeza lakini bahati nzuri mwenzetu Ibrahim Masoud Maestro alikuwa tayari na amesoma ukocha kwa hiyo alikuwa na uwezo wa kuongelea mechi kitalaam.

Baadaye ikatokea kozi ya waamuzi mimi (Alex) nikaingia ili kuufaham mchezo kwa kuzijua sheria 17 mwenzangu Shaffih akaingia kozi ya ukocha sasa hapo tukawa vizuri tukitaka kuzungumzia masulua ya maamuzi au kiufundi angalau watu wanajua ABC.

Boss Ruge akasema hicho ndio alikuwa anataka, msikilizaji anapata kitu cha ziada mbali na matokeo ya dakika 90. Tena akasema tusikariri kwamba kipindi ni lazima nusu saa tunaweza kwenda hata saa moja.

Kuanzia hapo tukawa tunafanya uchambuzi kwa kushirikisha na wadau wa nje pamoja na mashabiki.

Kama kuna radio zilikuwa na mfumo huo kabla ya Clouds basi zilikuwa chache sana, baada ya sisi kuingia kwenye mfumo huo sasa hivi ukifatilia karibu 80% ya radio zote Tanzania zipo kwenye mfumo wa uchambuzi wazo ambalo lilitoka kwa Boss Ruge.

Pia mbali na kuwa Boss alikuwa msikilizaji kama msikilizaji mwingine, hata ikitokea anakosoa anakwambia kabisa hapa nazungumza kama msikilizaji sio boss. Atakwambia jana nimesikiliza kipindi lakini timu fulani hamkuitendea haki kwa sababu kuna mambo 1, 2, 3, hamkuyazungumza.

Kwa hiyo wazo lake lilitoa fursa kwa wachambuzi kupata platform kwenye tasnia kwa sababu uchambuzi unafanywa na mtu yoyote sio lazima awe amesomea uandishi wa habari maana kabla wakati huo ilikuwa lazima uwe umesoma uandishi wa habari, una sauti nzuri na unaweza kutiririka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad