Samatta Amaliza Kazi na Kupaa Usiku wa Manane

Samatta Amaliza Kazi na Kupaa Usiku wa Manane
Usiku wa jana, Machi 24 imeshuhudiwa historia kubwa katika Uwanja wa Taifa ambapo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefuzu michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON baada ya miaka 39.

Hiyo ni baada ya kuifunga timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes" kwa mabao 3-0, mabao yaliyofungwa na Simon Msuva, Erasto Nyoni na Aggrey Morris.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ni miongoni mwa wachezaji waliocheza kwa kiwango cha juu katika mchezo huo, mara baada ya kumalizika kwa mchezo alikwea pipa na kurejea Ubelgiji katika klabu yake ya Genk huku akiacha ujumbe mzito kwa Watanzania.

Najivunia ubora uliooneshwa na wachezaji wenzangu,najivunia uwepo wa benchi la ufundi likiongozwa na kocha amunike, najivunia uwepo wa mashabiki waliojitokeza kutusapoti katika mchezo wetu wa jana na najivunia kuwa mtanzania na kapteni wa timu yangu ya taifa. Asanteni wote mliohamasisha na wote mliojotokeza kutusapoti

A post shared by Mbwana Samatta (@samagoal77) on Mar 24, 2019 at 4:42pm PDT

Pia wakati anaondoka katika Uwanja wa Ndege wa JNIA kuelekea Ubelgiji, majira ya saa 7 za usiku, Samatta aaliandika ujumbe, "mpaka wakati ujao, ahsanteni sana", ukionesha kuwa yuko safarini kurejea klabuni kwake.

Taifa Stars imeungana na timu ya taifa ya Uganda, Kenya na Burundi zitakazoiwakilisha Afrika Mashariki katika michuano ya AFCON itakayofanyika kuanzia mwezi June hadi Julai, 2019 nchini Misri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad