Wizara ya Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijijini ya Botswana imetangaza kuanza kutoa chakula cha asubuhi kwa wanafunzi wa shule za chekechea na shule za msingi nchini humo kuanzia mwezi ujao.
Tangazo hilo ambalo limeelezwa kuwa ni la haraka, limetolewa Machi 18 ambapo linasema kuwa wanafunzi hao wataanza kupewa bure chakula cha asubuhi kuanzia April Mosi kwaajili ya mwaka wa fedha wa 2019/2020.
Serikali ya Botswana imefikia uamuzi huo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na timu iliyoundwa mwaka 2013 kuwa wanafunzi wanatakiwa kupewa vyakula vyenye virutubisho ili kulinda afya zao, ukuaji na maendeleo pamoja na kupunguza magonjwa yatokanayo na upungufu wa lishe bora.
Chakula ambacho kinatarajia kutolewa ni pamoja na chai, mkate, 'peanut butter', mayai yaliyochemswa, uji, maziwa, machungwa na 'apple'.
Chakula hicho kimependekezwa kutokana na mahitaji ya virutubisho kwa wanafunzi, ambapo kitatolewa kwa wanafunzi hao kila siku asubuhi kabla ya kuanza masomo.
Hongera Botswana na sisi tutafikia huko Mungu atatujalia
ReplyDelete