Serikali Kufadhili Miradi 47 kuendeleza Ubunifu Nchini

Serikali Kufadhili Miradi 47 kuendeleza Ubunifu Nchini
Serikali imesema kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ipo katika mchakato wa kufadhilli Jumla ya miradi 47 ya kuendeleza ubunifu yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.4

Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh.William Ole Nasha ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua maonyesho ya kilele cha mashindano ya kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu ya mwaka 2019 ambapo amesema kuwa Matokeo ya miradi hiyo itachangia maendeleo ya Tanzania ya viwanda


 Aidha pia Mh.Ole Nasha amewashauri wabunifu nchini pale wanapofanya ubunifu kulinganisha jitihada zao na mahitaji ya wananchi ili ubunifu wao uweze kutatua changamoto mbalimbali zilizomo kwenye jamii

Pamoja na hayo pia ametoa rai kwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Tume ya sayansi na Teknolojia kutafuta namna ya kuwachukua washiriki wote waliofika katika hatua hiyo ili kuweza kuziendeleza kazi zao badala kuishia  kwa wale wachache watakao shinda pekee

 Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo James Mdoe amesema lengo mahususi la mashindano hayo ni kuibua na kutambua ubunifu na teknolojia mahiri zinazozalishwa na viijana wa kitanzania,kukuza hamasa ya ubunifu nchini na kuhamasisha maumizi ya sayansi,Teknolojia na ubunifu katika shugthuli mbalimbali za kijamii


 Mhandisi Peter Chisawilo yeye ni mbunifu na Mkurugenzi wa kampuni ya kubuni,kuunda na kuuza mashine na mitambo ya kusindika mazao ya kilimo akizungumza katika maonyesho hayo  amesema mtaji mkubwa wa mbunifu ni changamoto zilizopo kwenye jamii hivyo kuwashauri wabunifu kuzitumia vyema kubuni vitu vitakavyoenda kutatua changamoto hizo

 Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh,Joyce Ndalichako Novemba 14 Mwaka 2018 wakati alipozindua muongozo  wa kitaifa wa kutambua na kuendeleza ugunduzi,ubunifu na maarifa asilia ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Kukuza ujuzi na ubunifu kwa uchumi wa viwanda”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad