Show ya Nicki Minaj Imeahirishwa Tena, Cardi B Atajwa


Jumapili ya February 9,2019 Rapper Nicki Minaj aliahirisha show yake nchini Ufaransa tatizo likitajwa ni la kiufundi (mitambo ya sauti) na hivyo kupitia ukurasa wa instagram aliomba radhi kwa mashabiki kutokana na show hiyo kutofanyika.

Kwa upande mwingine wa mashabiki walionekana kutokubaliana na msamaha huo uliotolewa na Nicki Minaj na hivyo kuanzisha fujo nje ya hoteli alipofikia Rapper huyo na kuanza kulitaja kwa nguvu jina la Cardi B ambaye anahusishwa kuwa na ugomvi kwa muda mrefu na Nicki Minaj.

Inaelezwa pia  February 22,2019 Nicki Minaj aliahirisha show yake mjini Bratislava nchini Slovakia kwa matatizo ya kiufundi pia lakini Nicki Minaj ametoa sababu nyingine na kusema kuwa eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kufanya show lilionekana kutokuwa na umeme wa kutosha.

“Naenda chini kuona mashabiki zangu,jengo au Juice Wrld hawakutaka nifanye show usiku wa leo, walituacha tufanye majaribio ya sauti na wakasema jengo halina umeme wa kutosha kufanya show iendelee, kaeni tayari kupokea barua rasmi kutoka kwa promoters , Naombeni msamaha”Nicki Minaj

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad